Waziri Mchengerwa akutana na UNESCO, aunda tume ya uanzishwaji wa chuo Kikuu cha Kiswahili
Na John Mapepele, Waziri wa Utamaduni, Sanaa Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amekutana na ujumbe wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) na ameunda tume kwa ajili ya kuanzisha Chuo Kikuu cha Kiswahili nchini ikiwa ni mkakati kabambe wa kubidhaisha lugha ya Kiswahili katika mabara yote duniani. Mhe, Mchengerwa ameunda tume maalum ya uanzishwaji wa Chuo Kikuu cha Kiswahili kufuatia ombi lake alilolitoa kwa shirika la UNESCO wakati wa siku ya maadhimisho ya Kiswahili duniani mwaka huu iliyofanyika kwa mara ya kwanza Julai 7, 2022. Akizungumza mara baada ya mkutano na ujumbe wa UNESCO ofisi za Tanzania leo Agosti 5, 2022 ofisini kwake jijini Dar es Salaam amesema matajio ya Serikali ni kuona kuwa Kiswahili kinavuka mipaka ya Tanzania. Aidha, Mhe Mchengerwa ameipa tume hiyo siku tano kukamilisha andiko hilo ili liwasi...
Comments
Post a Comment